Mhe. Mkuu wa Wialaya ya Maswa Dr. Seif Shekarage ametoa salamu za serikalai kwenye Baraza la Madiwani la Robo ya Pili katika Halmashauri ya Wialaya ya Maswa.
Amegusia idara mbalimbali wakati wa kutoa salamu hizo kwa wananchi Wilaya hapa.
Kuhusu elimu ametoa shukrani kwa wataalamu, wah. Madiwani na wananchi kwa ushirikiano uliofanyika mwaka 2018 hadi kufanikisha ufaulu wa Wanafunzi kuwa mzuri. Kutokana na ufaulu huo amesema imejitokeza changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa hivyo akahimiza ushirikiano wa kufanikisha ujenzi wa vyumba hivyo ili watoto waliokosa nafasi waanze masomo. Pia amesema zifanyike jitahada za ujenzi wa nyumba za walimu na vyoo kwa shule ambazo hazina ili kuweka mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia.
Kwa upande wa huduma za Afya amesisitiza wananchi kujiunga Mfuko wa bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa (iCHF). Hapo awali tulikuwa na CHF iliyokuwa inatumika katika kituo kimoja tu anapojiandikishia mwanachama tena kwa gharama ya 10,000/=, hivi sasa imeboreshwa gharama ya kujiunga ni 30,000/= kwa mwaka na mwanachama atatibiwa hospitali yoyote ya Serikali mahali ilipo huduma hii hapa nchini.
Kuhusu suala la kutii/ kuheshimu sheria amesema kila mwananchi anatakiwa kulifahamu hilo ili kusaidia kuishi bila bugudha yoyote katika jamii zetu. Kutokana na hili amewataka wananchi wote wanaofuga mifugo ndani ya eneo la mamlaka ya mji mdogo waihamishe kwani atakayekutwa anachungia katika eneo hili atachukuliwa hatua za kisheria.
Amesisitiza pia suala la usimamiaji na ulipaji kodi kwa kila anayehusika. Kila mwenye biashara yoyote anatakiwa kulipa kodi, kwa wale ambao hawalipi kodi TRA wanatakiwa kuchukua vitambulisho vya wajasiliamali.
Ametoa ushauri kutokana na hali halisi iliyopo sasa vibuniwe vyanzo vingine vya mapato ili kuinua pato la Halmashauri. Amewahasa wafanya biashara kulipa ushuru wa huduma kama taratibu zinavyotutaka.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.