Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge ameongoza Watumishi kutoka katika Idara mbali mbali Wilayani hapa kupanda Miti katika eneo la Ofisi yake ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Muungano itakayoadhimishwa hapo kesho tarehe 26/04/2023.
Katika eneo hilo ameweza kuongoza Watumishi kupanda aina mbali mbali za Miti. Zoezi lilikuwa ni uzinduzi wa zoezi linaloendelea hapo kesho. Akiongea na Watumishi hao baada ya kukamilisha zoezi la upandaji miti amewahimiza kuadhimisha sikuu hapo kesho kwa kila mmoja kupanda Miti katika eneo aloishi.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge akichimba shimo kwa ajili ya kupanda mti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Muungano katika eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge akipanda mti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Muungano katika eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya leo 25.04.2023
Afisa Ardhi Wilaya ya Maswa Ndg. Vivian Christian akipanda mti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Muungano leo tarehe 25/04/2023
Afisa Mazingira Wilaya ya Maswa Bw. Dutu Lubinza akipanda mti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Muungano katika eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya leo 25.04.2023
Afisa Tarafa, Tarafa ya Nhung'hu Bw. Saria akipanda mti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Muungano katika eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya leo 25.04.2023
Afisa Tarafa, Tarafa ya Mwagala Bw. James Hongoli akipanda mti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Muungano katika eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya leo 25.04.2023
Watumishi kutoka idara mbali mbali Wilayani Maswa wakipanda miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Muungano katika eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya leo 25.04.2023
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.