Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Dr. Seif Shekarage leo tarehe 19/3/2019 amefanya kikao na waendesha pikipiki na baiskeli mjini hapa ili kukumbushana masuala ya usalama katika kazi zao.
Amewakumbusha kupitia uongozi wao waweze kufahamiana ili kurahisisha kubaini watu wabaya kati yao. Pia amewataka kuwa makini na kuwatambua abiria wao pindi wanapotaka kutoa huduma kwa wateja wao, kama ikitokea mwendesha Bodaboda au Daladala kutokuwa na imani na abiria wake asisite kutoa taarifa polisi kwa hatua za kiusalama kuchukuliwa.
Kikao hicho amewakumbusha pia umuhimu wa kuchukua vitambulisho vya ujasiliamali ambapo wamekubaliana na kuahidi kufikia Mwezi April watakuwa wameishachukua wote.
Mwisho amewahimiza kusimamia sheria kwa ajili ya faida yao na ya abiria wao pia wakati wawapo kazini.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.