Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Maswa kwa kupata hati Safi iliyotokana na ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali CAG kwa mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni, 2021 kwa usimamizi mzuri wa mapato uliofanywa na Mkurugenzi Mtendaji, Mwenyekiti pamoja na waheshimiwa Madiwani.
Kafulila amesema katika Mkoa wa Simiyu Halmashauri zote zimepata hati Safi kwa sababu ya utendaji mzuri wa wakurugenzi na usimamizi bora wa Madiwani katika Halmashauri ndio ulioziwezesha Halmashauri hizo kuwa na hati Safi.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo katika kikao maalumu Cha Baraza la Madiwani Cha kujadili hoja na mapendekezo ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG kilichofanyika leo 27 Juni, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa.
Mhe. Mkuu wa Mkoa ameipongeza Halmashauri ya Maswa kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye ukusanyaji wa mapato na kuvuka lengo la Mkoa ambalo ni asilimia 100 kwa kukusanya zaidi ya asilimia 120 na hivyo kuongoza Kimkoa kwa ukusanyaji mzuri wa mapato ambao umefanywa na watumishi wote wa wilaya ya Maswa pamoja na waheshimiwa Madiwani.
Aidha Mhe. Kafulila amesema kuwa Kasi ya kushughulikia hoja za zamani katika halmashauri zimefanyika kwa Kasi hivyo amemuomba Mkurugenzi kuendelea na mwendo huohuo ili hoja hizo ziweze kumalizika kwa wakati
Mhe. Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuwa madeni yote ambayo Halmashauri inadaiwa na wazabuni wanatakiwa kulipa baada ya mwezi mmoja wa mwaka mpya wa fedha utakapoanza ili kufunga hoja pia amewashauri Halmashauri wanapokusanya fedha hizo za ziada wanatakiwa kupeleka katika mfuko wa wanawake, vijana na walemavu.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa Ndg. Simon Berege amesema tayari madeni hayo yameanza kulipwa ambapo shs. milioni 147,126,803.3 tayari zimelipwa na Halmashauri vilevile ameahidi kuendelea kulipa madeni yote ambayo yameainishwa kwenye ripoti ya CAG wiki mbili baada ya mwaka mpya wa fedha kuanza.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.