Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. David Kafulila leo Juni 9, 2022 amefanya ziara wilayani Maswa katika Kata ya Sola kwenye kiwanda Cha Sola Ginerry kuongea na viongozi wa Ushirika kutoka Kanda zote za Mkoa wa Simiyu ili kuona namna ya kukifufua kiwanda hicho.
Akiwa wilayani Maswa Mh. Kafulila ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Maswa mh. Aswege Kaminyoge, kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Maswa, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, wataalamu wa pamba Ofisi ya Mkoa, washauri wa pamba Mkoa, wajumbe wa bodi SIMCU, viongozi wa AMCOS kutoka Wilaya sita za Simiyu na wataalamu wa Ushirika kutoka Halmashauri ya Maswa.
Akizungumza na viongozi hao Mh. Kafulila amesema ushirika ni chombo muhimu sana kinahitaji viongozi waadilifu wenye uwezo wa kumsemea mkulima ili mkulima ajione yeye ni AMCOS na kina uwezo wa kuwasaidia wakulima wa pamba katika kuwainua na kumfanya mkulima afanye mambo makubwa zaidi ya uwezo wake, pamoja na kuwasilisha matatizo yao.
"Ushirika ni msingi wa kuleta maendeleo na Sio tu maendeleo lakini maendeleo ambayo ni jumuishi, maendeleo ambayo yanabeba walio wengi" amesema Mh. Kafulila.
Mh. Mkuu wa Mkoa amewaomba watumishi wa AMCOS wajiamini na kufanya kazi zao kwa weredi kwa kuweka Mazingira mazuri ya kutoa huduma zao ili wakulima waweze kukimbilia huko, kufanya vizuri zaidi katika mambo makubwa ikiwepo ujenzi wa maghala sehemu mbalimbali ili kufanya vitu vionekane ambavyo ni alama kwa AMCOS.
Ameongeza kuwa bodi ya pamba nchini ilitoa miongozo miwili na mmojawapo wa muongozo huo ni Simiyu model mfumo unashirikiana na serikali kuanzia ngazi ya Kijiji kwa kuunda kikosi kazi Cha pamba chenye lengo la kuhakikisha udhibiti na usimamizi wa uhakika kwenye sekta ya pamba ili mkulima alejeshe Imani kwa Ushirika kuwa bado ni dhana sahihi ya kumfanya asiye na kipato aweze kupata pembejeo, soko ambalo limelatibiwa ili aweze kupata kile anachostahili.
Kwa upande wake afisa mfawidhi maendeleo ya biashara kutoka benki ya kilimo ofisi ya Kanda Mwanza Ndg. Marko Samson amesema benki ya kilimo imetoa bilioni 6.5 kwa ajili ya kukarabati ginerry ya sola na kununua pamba, kuboresha uzalishaji kwa kuwapa wakulima matrekta na kuboresha uifadhi wa zao la pamba kwa kujengwa maghala ya kuhifadhia pamba.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.