Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Ndg. Simon Berege amewahaidi kuwapatia ushirikiano wa hali ya juu Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri hii katika shughuli zote za maendeleo wilayani hapa.
Akizungumza leo kwa mara ya kwanza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani amesema kuwa atatoa ushirikiano kwa viongozi wote Wilayani hapa katika shughuli mbalimbali za maendeleo ili kuhakikisha Wilaya hii inakwenda kasi zaidi ya hapo ilipofikia.
Aidha amewaomba Waheshimiwa Madiwani pia kumpatia ushirikiano ili kwa pamoja waweze kusukuma gurudumu la kuwaletea maendeleo wananchi wa Wilaya hii. Berege aliteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Maswa, kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala huko Kahama mkoani Shinyanga.
Ndani ya kikao cha Baraza hilo zimeibuliwa hoja mbalimbali na Waheshimiwa Madiwani likiwemo la Maji.
Diwani wa Viti maalum Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu Devotha Pingu ameiomba Mamlaka ya maji MAUWASA kutoa elimu kwa wateja wao jinsi ya kusoma namba za mita za maji ili kuepusha minong'ono kwani kumetokea na lawama juu ya usomaji wa mita na kuleta ankra kubwa bila kujua.
Amefikisha malalamiko hayo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Wilayani hapa kilochofanyika leo tarehe 25 October 2021.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji Maswa MAUWASA Raphael Mwita amekili kuwepo kwa tatizo la usomaji wa mita za maji na kuahidi kulishugulikia swala hili kwa uzuri zaidi ili kuwapa huduma nzuri wateja wao.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.