Leo tarehe 1/11/2019 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa amefanya kikao na Watumishi wa Kata saba Wilayani hapa. Katika kikao hicho Watumishi wamepata fursa kutoa kero na changamaoto wanazokutana nazo katika mazingira ya utendaji kazi. Waatumishi 405 wa Idara za Elimu Msingi na Sekondari, Afya, Fedha, Utawala, Kilimo, Mifugo, Maendeleo ya Jamii, Mipango, Mazingira na Ardhi; Vitengo vya Manunuzi, TEHAMA, Sheria, TSC na Udhibiti Ubora kutoka katika Kata za Binza, Mwamashimba, Nyalikungu, Ng'wigwa, Shanwa, Sola na Sukuma wamehudhuria kikao hicho.
Katika kikao hicho mambo mengi yahusuyo taratibu za kiutumishi yamelezwa. Kwa msisitizo Mkurugenzi Mtendaji amewaelekeza Walimu Wakuu, Wakuu wa shule na Wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya kutumia vema mapato wanayopata ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila mtumishi kwenye kituo husika anakunywa chai wakati awapo kazini.
Amesisitiza pia suala la kufikisha taarifa Ofisi ya Mkurugenzi lifuate utaratibu sahihi ili kupunguza mizunguko ya Watumishi wakati wa muda wa kazi na kurahisisha mawasiliano kwa kuagiza Walimu waandikapo Barua zao zisainiwe na kuwasilishwa kwa Mratibu Elimu Kata ambaye ataziwasilisha ofisi ya Afisa Elimu huku Mhudumu kutoka Ofisi ya Elimu akifikisha katika Masjala ya Halmashauri tayari kufika kwa Mkurugenzi vivyo hivyo kurudi kwake. Kwa hilo Barua zote kutoka ngazi ya chini zisizidi siku tano kuwa zimefika hadi kwa Mkurugenzi na kufanyiwa kazi. Wajumbe wamepokea maelekezo hayo na kaahidi kuyatekeleza.
Aidha katika ufafanuzi wa maelekezo amesisistiza kila kituo cha kutolea huduma kufanya vikao vya kupanga matumizi ya Fedha Watumishi wote wa kituo husika ili kuweka uwazi na uwajibikaji kwa kila mmoja hapo kituoni.
Katika hatua ya kujibu kero mbalimbali Mkurugenzi Mtendaji na Wakuu wa Idara mbalimbali wametoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kiutumishi ikiwemo na ufuatiliaji wa stahiki za Watumishi.
Pia Mkurugenzi Mtendaji ametumia fursa hiyo kuwapongeza Walimu wote wa Shule za Msingi Wilayani hapa kwa kazi nzuri waliofanya na kufaulisha Wanafunzi wengi ambapo ufaulu huo umeiwezesha Wilaya kutoka nafasi ya 100 mwaka 2018 na kupata nafasi ya 42 mwaka 2019 Kitaifa.
Mwisho amewahasa Watumishi kufanya kazi kwa kufuata taratibu, sheria na kanuni na pale wanapopata changamoto wasisite kutoa taarifa katika Mamlaka husika yaani kufikisha kwa Mkuu wa Idara na ikishindika mtumishi hana budi kufikisha moja kwa moja kwa Mkurugenzi Mtendaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.