Halmashauri ya Wilaya ya Maswa leo imesaini mkataba wa ufundi wa ujenzi wa jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, ujenzi ambao utatekelezwa kwa awamu tatu ambapo katika awamu hii ya kwanza serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.
Aidha ujenzi huo utatekelezwa kwa kutumia force account ambapo fundi atakayetekeleza ujenzi huo ni fundi ujenzi( local fundi ) Berno Batinamani ambaye ameshinda dhabuni hiyo kupitia mfumo wa manunuzi (TANEPS) na ujenzi huo unatakiwa kukamilika kwa miezi sita.
Mkataba huo umesainiwa katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa na kushuhudiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mhe. Paul Maige, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg. Maisha Mtipa pamoja na wakuu wa Divisheni na Vitengo leo tarehe 23/09/2023. Jengo hilo litajegwa katika Kijiji cha Ng'hami Kata ya Nyalikungu.
Baada ya kusaini na kukabidhiana mkataba huo, fundi ameenda kuonyeshwa eneo la ujenzi tayari kwa kuanza kazi.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.