Leo MAUWASA imefanya kikao na wadau pamoja na watumiaji wa maji Wilayani Maswa kuhusu ombi la kurekebisha bei ya majisafi.
Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Maswa ni mradi wa Maji wa Kitaifa miongoni mwa miradi 8 ya Maji ya Kitaifa iliyoko Tanzania Bara. Miradi mingine ya kitaifa ni KAHAMA SHINYANGA (KASHWASA), Handeni Trunk Main (HTM), Chalinze (Pwani), Mugango /Kiabakari (Mara), Masasi-Nachingwea, Makonde (Mtwara) na Wanging’ombe (Njombe). Mradi wa Maji Maswa unahudumia mji wa Maswa na vijiji 11 vya Zanzui, Malita, Dodoma, Mwabayanda, Mwasita, Mwabujiku, Hinduki, Buyubi, Mwadila, Iyogelo na Ng’wigwa.
Awali Mamlaka hizi gharama zake za uendeshaji na matengenezo zilikuwa zinachangiwa na Serikali hasa kulipa mishahara ya watumishi na kulipia bili za umeme. Lakini kwa sasa Mamlaka hizi zimetakiwa kujitegemea.
Gharama za huduma za majisafi zinazotumika kwa sasa zilipitishwa mwaka 2009 na tangu hapo mbali na gharama za vipuli, umeme, mabomba na viungio vyake, madawa ya kutibu maji, bidhaa za petrol kupanda mwaka hadi mwaka gharama hizi zimebaki palepale.
Kufuatia mabadiliko haya gharama zinazotumika sasa zinashindwa kukidhi gharama za uendeshaji na matengenezo pamoja na uwekezaji mdogomdogo. Aidha, Mamlaka inatakiwa kuanza kujitegemea kwenye gharama zote za uendeshaji zilizokuwa zikichangiwa na Serikali ili kuiacha Serikali kuendelea na uwekezaji katika miradi mipya.
Kwa maelezo zaidi soma Taftishi kuhusu ombi la mabadiliko ya bei.pdf na Tangazo la EWURA.pdf
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.