Kamati ya mradi wa uboreshaji miji mjini na vijijini kutoka wizara ya ardhi imetoa mafunzo kwa wajumbe wa CMT katika Halmashauri ya Maswa wenye lengo la kupanga, kupima na kumilikishwa ardhi ili kuepuka migogoro pamoja kuwe na matumizi sahihi ya ardhi kwa wananchi wa maeneo hayo ya vijiji.
Akizungumza katika kikao hicho mjumbe wa kamati ya uboreshaji miji mjini na vijijini kutoka wizara ya ardhi Ndg Paul Samwel amesema Mradi huu unatekelezwa na serikali baada ya kupata mkopo kutoka Benk ya Dunia ambapo fedha hizo zitatumika kutekeleza mradi huo katika Mikoa 15, Halmashauri 41 kati ya Halmashauri hizo 34 ni Halmashauri za miji/ manispaa na Halmashauri za Wilaya 7.
Halmashauri ya Maswa ni miongoni mwa Wilaya ambazo mradi wa matumizi sahihi ya ardhi umefika kwa mantiki ya kuwepo kwa mipango miji kutokuwepo kwa migogoro mingi ya ardhi na maeneo mazuri ya uzalishaji ikiwepo kilimo imechagiza mradi huu kufika Maswa
Mpango huo wa matumizi ya ardhi ya Wilaya utawezesha kubaini matumizi sahihi ya ardhi kabla ya kuandaa matumizi ya ardhi ya vijiji ambao kubaini mipaka na aina mbalimbali za makundi ya ardhi yaliyopo katika hifadhi ya Wilaya ya Maswa ili kuepusha migogoro kwa kuwa swala hili ni shirikishi kwa wananchi wote
Mradi utakuwa na malengo ambayo ni uboreshaji wa usalama wa miji kwa kupima takribani viwanja 50,000 katika vijiji 250 kwa Halmashauri saba na Maswa ikiwepo, uboreshaji wa mifumo ya kidigitali katika ofisi za wizara kwa kuanzisha mfumo unganishi wa taarifa za ardhi (intergrated land information system) pamoja na ujenzi wa majengo ya gorofa moja katika mkoa kwa ajili ya ofisi.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii mwandamizi kutoka wizara ya Ardhi Ndg. Tumaini Situmbi amesema Mradi huu unazingatia sana haki za binadamu katika utekelezaji wake hivyo amewataka wajumbe wanaohusika kwenye mazingira na maendeleo ya jamii kutoa Elimu ya kutosha kwa wananchi ili wawe na uelewa wa kuhusu mradi na kuhamasisha.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.