Mradi wa BOOST ni mradi unaokuja kwa ajili ya kuinua elimu ya Awali na Msingi. Mradi huu utahusisha masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa miundombinu (Madarasa), Ununuzi wa Vifaa vya TEHAMA, Mafunzo kwa walimu n.k Mafunzo ya Mradi huu katika Kanda ya Magharibi iliyojumuisha Wataalamu kutoka katika Halmashauri 20 za Mikoa ya Tabora, Simiyu na Shinyanga yamefanyika katika Chuo cha Ualimu Tabora kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 16-17/12/2022.
Kila Halmashauri ilikuwa na Wajumbe 13 na kila Mkoa Wajumbe 8. Mradi unatekelezwa kwa Mpango wa lipa kwa matokeo (EP4R).
Lengo kuu la Mradi ni kuboresha upatikanaji wa fursa katika ufundishaji na ujifunzaji bora wa elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara. Mpango kazi unatekelezwa katika afua kuu nane ambazo ni:-
1. Miundombinu
2. Mpango wa shule Salama
3. Kuongeza udaili kwa Watoto wa Awali
4.Kuongeza upatikanaji wa Vifaa vya kufundishia na kujifunzia elimu ya Awali
5.Mafunzo Endelevu ya Walimu kazini (MEWAKA)
6. Kuimarisha matumizi ya Mifumo ya TEHAMA katika ujifunzaji na ufundishaji
7. Kuimarisha Mipango na Bajeti
8. Kuwajengea uwezo viongozi na umahiri katika kazi
Akihitimisha Mgeni Rasmi amesema ili kutekeleza mradi kama malengo yanavyotaka, ushirikiano ni wa lazima kwa kila mjumbe wa timu ya utekelezaji. Pia amewataka Wahasibu, Wahandisi na Maafisa Manunuzi kuwasaidia Walimu wanaosimamia miradi hasa katika suala la malipo na manunuzi ili miradi yetu ikamilike vizuri kukiwa na nyaraka sahihi kama zinavyotakiwa. Amesisitiza Halmashauri kwenda kusimamia na kutekeleza Afua zote kulingana na vigezo ili mradi wetu ukawe wa mfano kitaifa katika Kanda yetu.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.