SALIKI kirefu chake ni Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji, hufanyika mara moja kwa kila robo kwa kila Kijiji, shughuli mbalimbali hufanyika siku hio kama vile utoaji wa elimu ya lishe kwa nadharia na vitendo, upimaji wa hali ya lishe kwa watoto wenye umri wa miezi 0 hadi 59. Kwa wiki hii yote tunaadhimisha kwenye Kata tatu za Kadoto, Shishiyu na Jija zenye jumla ya vijiji 11, elimu ya lishe imetolewa kwa nadharia na vitendo, watoto walipimwa hali ya lishe. Uji ulipikwa kwa kutumia makundi 5 ya chakula, tulitumia unga wa sembe, maziwa, Karoti, ukwaju na sukari. Shughuli hii inafanyika kwa ushirikiano na shirika la World Vision AP ya Shishiyu.
Pia tumeunganisha na zoezi la mwezi wa Afya na Lishe ya mtoto ambapo Watoto wanapimwa hali ya lishe na kupewa matone ya vitamin A pamoja na dawa za kuzuia maambukizi ya minyoo.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.