• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Mrejesho |
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini ya Mjini
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Uratibu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Tehama
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria ndogo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa aipongeza Maswa

Posted on: July 11th, 2022

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa  Uhuru kitaifa mwaka 2022  Ndg.  Sahili Geraruma  ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Maswa kwa kutenga eneo la uwekezaji kwa ajili  ya uwezeshaji wa vikundi  vya vijana, watu wenye ulemavi na wanawake ili waweze  kufanyia shughuli zao za maendeleo ya kiuchumi.

Akizungumza wakati  wa uwekaji jiwe la msingi eneo la uwekezaji lenye thamani ya shs 55,785,096.60 katika kiwanda Cha mikate lishe kilichopo Kijiji Cha  Ng'hami, Kata ya Nyalikungu leo tarehe 11 julai 2022 kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa amesema Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imeupiga mwingi katika suala zima la uwekezaji kwa kuanzisha viwanda na miundombinu yote inayohitajika katika uwekezaji ikiwepo umeme na maji.

"Mradi ni mzuri pongezi kubwa sana kwa Mkurugenzi mtendaji, kazi nzuri umefanya" amesema Geraruma.

Katika hatua nyingine Mwenge wa Uhuru  umezindua mradi wa ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa katika Shule ya Sekondari Ipililo Kijiji Cha Ipililo wenye thamani ya shs 91,941,000/=  uwekaji jiwe la msingi katika jengo la wagonjwa wa dharura hospitali ya wilaya ya Maswa uliaogharimu shs 300,000,000/=, mradi wa ujenzi wa Tanki la maji katika kata ya Nyalikungu  wenye thamani ya shs 497,372,690.40 pamoja na ujenzi wa Barabara ya kiwango Cha lami kilomita moja uliogharimu shs 499,999,270/=.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa ameipongeza wilaya ya Maswa kwa kuwa Mwenge wa Uhuru umepitisha miradi yote na amewaomba viongozi wote kushirikiana kuanzia ngazi ya chini mpaka juu kwa ajili ya maendeleo ya Maswa.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Mwenyekiti wa kamati ya huduma na maendeleo ya jamii, pia mjumbe wa Halmashauri  kuu ya CCM Taifa Mh. Stanslaus  Nyongo  amempongeza  Mh.  Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa zaidi ya shs bilioni 30 kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo katika Wilaya ya  Maswa katika mwaka huu wa fedha.

Aidha Geraruma amewaomba wananchi wa wilaya ya Maswa  kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi litakolofanyika Augusti 23, 2022 ili serikali iweze kujua takwimu sahihi ya idadi ya watu kwa ajili ya utekelezaji wa dira ya maendeleo ya mwaka 2025, "Sensa ni msingi wa mipango ya maendeleo shiriki kuhesabiwa tuyafikie maendeleo ya taifa".

Awali akipokea Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Mbugamita Kata ya Senani ukitoka Wilaya ya Meatu Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh. Aswege Kaminyoge alisema mwenge wa uhuru utakimbizwa Kilomita 153 kukagua miradi mitano katika Wilaya ya Maswa.




Matangazo

  • TANGAZO LA UHAMASISHAJI CHANJO YA MIFUGO January 21, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI May 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI May 27, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO May 30, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA YATOA MAFUNZO YA MFUMO WA NeST KWA WATAALAMU WA UNUNUZI WILAYANI MASWA

    March 27, 2025
  • DKT ANNEY; NENDENI MKASIMAMIE MIRADI YETU VIZURI

    March 26, 2025
  • VIKUNDI 15 VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYAPATA MKOPO

    March 26, 2025
  • KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO MASWA

    March 10, 2025
  • Tazama zote

Video

Fursa za uwekezaji Mkoani Simiyu
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Sensa ya mwaka 2022
  • Taarifa ya Mapato na matumizi
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa IMIS
  • Mfumo wa PlanRep
  • Government Web Framework
  • Mfumo wa PREM
  • Maswa DC Mail Domain
  • Hotuba ya Mh. Waziri Mkuu PLANREP/FFARS

Viunganishi linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Sekretariet ya Ajira
  • Ikulu
  • Baraza la Mitihani Tanzani
  • Wizara ya Elimu Tanzania
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

    Sanduku la Posta: 170, MASWA

    simu ya Mkononi: +255 282 750 271

    Simu: +255 282 750 271

    Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.