Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu Mkoa wa Simiyu Ndg John M. Tilubuzya amewataka waandishi waendesha ofisi kutembea kifua mbele kwa kujiamini, kwa sababu serikali inatambua umuhimu wao katika utendaji kazi.
Akizungumza wakati akifungua kikao hicho cha waandishi waendesha ofisi (PS) kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa leo tarehe 05. 05.2023 na kuudhuriwa na waandishi waendesha ofisi 40 kati ya 67 kutoka katika Wilaya zote za Mkoa wa Simiyu.
“Katika utumishi wa umma kada yenu ni kada muhimu sana na kutokana na umuhimu huo ndio maana hata Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan ameona ni bora kukutana na nyie, Ukipata mwaliko wa Mhe. Rais wewe ujue wazi kabisa una umuhimu mkubwa katika uendeshaji wa shughuli za serikali”. Amesema Tilubuzya
Ndg Tilubuzya amewapongeza SIPSEA kwa ushirikiano ambao wameuonyesha kwa kuanzisha chama chao ambacho wamekisajili ili kiwasaidie kwenye mambo mbalimbali katika kutatua changamoto walizonazo ikiwemo misiba na sherehe.
Katibu tawala msaidizi sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu ametoa wito kwa wanachama wote kushirikiana katika kutoa michango kila mwezi kama ilivyo ada na wale wote walio katika kada hiyo ambao hawajajiunga katika chama hicho watoe michango ambayo itasaidia mwanachama yeyote atakayepata shida kusaidiwa kwa urahisi ili kudumisha umoja huo.
Ndg Tilubuzya hajaridhishwa na maudhurio ya waandishi waendesha ofisi hao ambapo amewaahidi ataongea na wakurugenzi wa wilaya ili kuwaeleza picha harisi kwa kuwa hata nusu yao hawakufika na kujua sababu zilizosababisha watumishi hao wasihudhurie kikao hicho.
Awali akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Katibu wa Umoja wa Waandishi Waendesha Ofisi Mkoa wa Simiyu (SIPSEA) Loyceah J Ishengoma amesema umoja huo ulianza 29 Aprili, 2019 ukiwa na wanachama 32 ambapo mpaka sasa wapo wanachama 67
Ishengoma amesema lengo la kuanzisha chama hicho katika Mkoa wa Simiyu ni kuwaunganisha pamoja waandishi waendesha ofisi, kuwa na umoja imara, kusaidiana kwenye shida na raha ikiwemo misiba na sherehe.
Aidha amesema kuwa kutokana na changamoto wanazokutana nazo wameomba kupatiwa mafunzo ambayo yatawajengea uwezo kwa kuwezeshwa fedha, kupewa vibari na waajiri wa taasisi mbalimbali kwa ajili ya mafunzo ya kitaaluma ndani na nje ya Mkoa.
Kikao hicho kinafanyika ikiwa ni ratiba ya chama hicho kukutana kila mwaka kujadili mambo mbalimbali yaliyotekelezwa kwa mwaka uliopita, kupata taarifa ya mapato na matumizi pamoja na kutatua changamoto ambazo hazijapatiwa ufumbuzi katika maeneo ya kazi.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.