Leo tarehe 19/1/2018 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Ndg. Jumanne A. Sagini amefanya kikao maalumu na wadau wa elimu katika ukumbi mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kilicholenga suala zima la kusimamia taaluma ili kuinua kiwango cha elimu.
Kikao kimejumuisha Wakuu wa Idara, Maafisa Elimu Wilayani na Kata, Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu Wilayani Maswa. Kiongozi huyu amewataka wakuu wa Idara na Vitengo kuwa na ushirikiano wa pamoja katika kusimamia suala zima la elimu Wilayani Maswa ili kuinua kiwango cha ufaulu.
Amesema “pamoja na wingi wa wanafunzi, uchache wa walimu, mwitikio hafifu wa Wazazi katika suala la elimu hapa Wilayani, changamoto hizi zote na nyinginezo zisitufanye tubweteke bali tunatakiwa kujipanga kusimamia suala zima la elimu kwa kutumia taaluma tulizonazo”. Amesisitiza walimu wasimamie taaluma na siyo kazi nyingine.
Amewataka Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu wawachukulie hatua / wawajibishe Walimu walevi, watoro na wasiofundisha ipasavyo kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni za kazi. Ameongeza kwa kusisitiza kuwa Watumishi walevi, watoro kazini na wasiotimiza wajibu wao siyo rahisi kupandishwa daraja / cheo pamoja na watumishi wanaowajibika.
Aidha Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu amewaagiza Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu wasio na kipindi hata kimoja cha kufundisha kwa wiki kuanzia sasa wawajibike pia kufundisha. Ameenda mbali kwa kuwataka Maafisa Elimu Kata pia wapate muda wa kwenda kufundisha.
Kwa kupiti kikao hiki Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu Ndg. Julius Nestory ametoa maagizo yafuatayo:
Katika kuhitimisha Katibu Tawala Wilaya ya Maswa Ndg. Rutalemwa P. Rutagumirwa amesema kila Mwalimu atimize wajibu wake ili kuweza kuinua kiwango cha elimu Wilayani Maswa. Amesisitiza kwa kauli mbiu hii “Kwa pamoja tuseme tutabadilika na tutaleta mageuzi ya Elimu, hivyo ufaulu utaongezeka Wilayani Maswa”
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.