Wajumbe wa kamati ya Lishe Wilaya ya Maswa wamefanya ziara katika kiwanda cha kusindika ungalishe kilichoko katika kijiji cha Njiapanda Kata ya Isanga Wilayani Maswa.
Katika ziara hiyo hapo kiwandani wamepata maelezo toka kwa mtaalamu wa tekinolojia ya chakula ya kuwa kabla ya kupata unga wa viazi lishe kuna hatua mbalimbali zinazopitiwa; ambazo ni
(i) Mapokezi ya viazi kutoka kwa Wakulima
(ii) Uchambuzi wa viazi vinavyofaa (Sorting)
(iii) Kuosha viazi (Cleaning)
(iv) Kutengeneza michembe (Slicing)
(v) Kukausha michembe (Drying)
(iv) Kusindika au kusaga unga (Processing)
(vii) Kufungasha unga kwenye mifuko (Packaging)
Aina za Unga unaozalishwa katika kiwanda hiki
Wajumbe wa kamati ya lishe kwa kushirikiana na Idara ya Kilimo wameombwa kuhamasisha kilimo cha mazao ya ufuta, ulezi na maboga ambayo kuanzia mwezi wa Oktoba malighafi huwa ya shida kupatikana kwa sababu ni wakulima wachache wanaolima mazao hayo.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.