Kamati ya Elimu Afya na Maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imewataka watendaji wa Halmashauri hiyo kusimamia kwa karibu miradi inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Maswa kwa kuwa Bado asilimia kubwa imechelewa kukamilika baada ya kamati hiyo kutembelea na kufanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa hapa Wilayani.
Kamati imetembelea miradi minne ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata ambayo ni ujenzi wa nyumba ya mtumishi katika zahanati ya Mwabayanda Kata ya Ng'wigwa mradi unaosimamiwa na TASAF, ujenzi wa madarasa mawili na ofisi moja katika shule ya Sekondari Mwakaleka Kata ya Binza, ujenzi wa majengo mawili katika kituo Cha afya Shishiyu ikihusisha jengo la upasuaji (theatre), jengo la wazazi (maternity), pamoja na madarasa mawili, ofisi moja na choo matundu sita katika shule ya msingi Mwabujiku Kata ya Zanzui.
Ziara hii ya wajumbe imefanyika ikiwa ni ukaguzi wa utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Elimu, Afya na Maji kuona namna ambavyo miradi inatekelezwa.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa kamati ya Elimu, Afya na Maji wamewaomba wataalamu kusimamia kwa karibu miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati kwa kutatua changamoto zinazojitokeza ikiwepo ukosefu wa maji na kulipa mafundi na kushirikiana kwa karibu na watendaji wanaosimamia miradi hiyo
Wataalamu wamepokea maelekezo yote na wameahidi kusimamia kwa karibu kwa kuwa changamoto ya mfumo imemalizika hivyo miradi yote itaisha kwa wakati na wananchi watafaidika kwa kuwa huduma zitaanza kutolewa.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.