Mganga Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dk Hadija Zegega amezindua chanjo ya surua, lubela kwa lengo la kuwalinda watoto wenye umri chini ya miaka mitano kuepukana na magonjwa hayo.
Hayo yamesemwa leo tarehe 15.02.2024 mwaka huu wakati akizindua chanjo hiyo katika hospitali ya Wilaya ya Maswa amsema Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu inatarajia kuwapatia chanjo ya ugonjwa wa surua na rubella watoto wapatao 110,891 wenye umri chini ya miaka mitano ili kuweza kujikinga na magonjwa hayo.
Amesema mpango wa Halmashauri ya Wilaya kupitia Divisheni hiyo imepanga kuwafikia watoto hao ili kuhakikisha kila mmoja anapatiwa chanjo hiyo ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya kuwalinda ili wasiweze kupata magonjwa hayo.
"Mpango wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ni kuwafikia Watoto110891 kwa kipindi cha siku nne kuanzia leo februari 15 hadi februari 18 mwaka huu na tukiwachanja wote hao tutakuwa tumefikia lengo letu la kuwachanja watoto kwa asilimia 100 waliopo katika wilaya ya Maswa,"amesema.
Dk Zegega amesema ili kuweze kufikia malengo hayo ni vizuri Wakinamama wenye watoto wenye umri huo kuwapeleka watoto wao katika vituo vya kutolewa chanjo ili waweze kupaya chanjo hiyo ili kuwakinga na ugonjwa wa surua ambao unaweza kumsababishia mtoto upofu na madhara kwenye mapafu.
"Napenda kutoa rai kwa akinama wenye watoto wenye umri wa miezi tisa hadi miezi 59 kuwapeleka watoto wao katika vituo vya kutolea chanjo ili waweze kupata chanjo hii ya surua na rubella kwani ugonjwa wa surua ni hatari kwa watoto unaweza kumsababishia upofu pamoja na madhara kwenye mapafu,"amesema.
Awali Mratibu wa Chanjo wilaya ya Maswa, Abel Machibya amesema kuwa Hospitali ya Wilaya hiyo ni miongoni mwa vituo 102 ambavyo vitatoa chanjo hiyo ili kuhakikisha watoto wote waliowekwa kwenye lengo la kuchanjwa wanafikiwa.
Amesema kuwa chanjo hiyo ni bora na salama kwa afya za watoto hivyo ni vizuri wananchi wote wakajitokeza kwa wingi kuwaleta watoto wenye umri huo katika vituo vya huduma na huduma ya mkoba kwa ajili ya kupata chanjo hiyo muhimu kwa afya ya watoto wao.
"Tutakuwa na vituo 102 kwa ajili ya kutolea chanjo hii ya Surua na Rubela na kituo cha hospitali ya Wilaya ya Maswa ni miongoni kati ya vituo hivyo ninawakaribisha wakinamaa wenye watoto wenye umri huo wawalete watoto wao ili wapate chanjo hiyo ambayo ni salama,"amesema.
Pia, amewaasa watumishi wa kada ya afya kutoa huduma kwa kufuata misingi ya viapo vyao na kwa uadilifu na uaminifu ili wananchi wa Maswa washuhudie ubora wa huduma lakini pia thamani ya wanaotoa huduma hizo.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.