Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Balozi, Dkt Emmanuel Nchimbi amewapongeza wananchi wa Maswa kwa kushiri katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani Maswa.
Dkt Nchimbi ametoa pongezi hizo wakati akiongea na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Madeko Wilayani Maswa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM.
"Nawapongeza wananchi kwa kutoa ushirikiano kwenye miradi iliyofanyika maana bila nyinyi kutoa ushirikiano miradi hiyo isingefanikiwa." amesema Katibu Mkuu
Aidha Katibu Mkuu ameupongeza uongozi wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, Wenyeviti wa Halmashauri na Waheshimiwa Madiwani kwa kazi kubwa wanayoifanya katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Pia Dkt Nchimbi amewapongeza wabunge wote kwa kushirikiana na serikali kutekeleza miradi hiyo, pia ameipongeza Halmashauri na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha Fedha hizo ili kufanikisha miradi hiyo.
"Hivi ndivyo tunataka nchi yetu iendelee mambo ya msingi ya wananchi wetu, afya zao, Elimu ya watoto wao, barabara Bora, usalama wa raia wetu hayo ndio mambo yanayosimamiwa na serikali inayojitambua na Rais wetu kwa miaka mitatu na nusu ameonyesha kwa vitendo jinsi ambavyo anajali Maisha ya watanzania wetu." Ameeleza Dkt Nchimbi
Pia ameongeza kuwa Rais anatafuta Fedha usiku na mchana kuhakikisha kwamba watanzania wanahudumiwa vizuri pamoja na kusimamia ngazi mbalimbali ili kuhakikisha Fedha zinafika kuhudumia wananchi.
Katika hatua nyingine Dkt. Nchimbi amewataka wananchi wa Maswa kulinda amani iliyoasisiwa na wazee wa nchi hii akiwemo baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abed Karume .
Pia katibu Mkuu ametumia mkutano huo kuwashukuru wazee wote kwa kujenga Taifa ambalo mpaka Sasa limekuwa na umoja, amani na mshikamano
"Wajibu tulionao sisi watu wa umri wangu na kuendelea chini ni kufanya jitihada kubwa kuhakikisha kwamba tunailinda amani, umoja na mshikamano ambao wazee Hawa wametuachia. Ameeleza Dkt Nchimbi
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.