Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg. Maisha Mtipa ameahidi zawadi ya pikipiki mbili kwa Mwalimu Mkuu na Mwalimu atakayefaulisha mtihani wa darasa la saba mwaka 2024 kwa wastani "A"
Ndg. Mtipa aliyasema hayo katika kikao cha cha kutathimini matokeo ya mtihani wa Mock kanda ya ziwa kilicchowashirikisha umoja wa wakuu wa shule za msingi Wilaya ya Maswa ambacho kilifanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Lengo la kikao hicho ni kutathmini matokeo ya mock, mbinu na mikakati ambayo itafanyika ili kuongeza ufaulu katika mtihani wa darasa la saba na mitihani mingine.
Pia Mkurugenzi Mtendaji aliwapongeza Walimu wote kwa matokeo mazuri waliyoyapata katika mtihani wa kujipima ( mock) kanda ya Ziwa ambapo ufaulu umepanda na kufikia asilimia 86 mwaka huu.
"Mwaka jana ufaulu ulikuwa asilimia 79 lakini Mock tumeanza kufika kwenye maeneo ambayo tulikuwa tunayasema asilimia 85 kwa hiyo mimi niwatie shime bado tuendelee kupambana licha ya idadi ya watu waliokuwepo,"
"Tukifika katika ile asilimia kuliyokubaliana mwaka jana ya asilimia 85 ile ahadi tena itajirudia, nia yangu kubwa ya kuja hapa ni kurudia kauli yangu ya mwaka jana tukifika asilimia 85 kwenye tathmini yetu basi ile ahadi yangu ya kuwapeleka Serengeti nitaitekeleza tena ." Alisema Mkurugenzi Mtendaji
Aidha Ndg Mtipa alitoa pongeza kwa Walimu kwa kazi ngumu waliyoifanya licha ya changamoto wanazokutana nazo katika mazingira ya kazi lakini wanapambana ili kusukuma gurudumu la uboreshaji wa elimu.
Awali akitoa taarifa Afisa Elimu ya msingi Wilaya ya Maswa Dkt lucy Kulong’wa alisema Wilaya ya Maswa imefanya vizuri katika mtihani wa mock darasa la saba kwa kuwa ufaulu umepanda kwa asilimia 4.33 kutoka asilimia 80.9 mwaka 2023 na kufika asilimia 85.2 mwaka huu.
Pia Dkt Kulong"wa alisema Wilaya ya Maswa imeshika nafasi ya tisa kikanda kati ya mikoa 5 ya Kanda ya Ziwa na kimkoa imeshika nafasi ya tatu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa tapsa Wilaya ya Maswa, ambaye pia ni Mwalimu Mkuu shule ya msingi Shanwa Mwalimu Mbaga Shilla alishukuru kwa kikao hicho ambacho kimewapa mbinu na mikakati mbalimbali ya kuongeza ufaulu kwa sababu kila mwalimu Mkuu atafanya jitihada kuhakikisha kuwa matokeo yanakuwa mazuri.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.