Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge amewapongeza watendaji wa kata,vijiji na viongozi wa kuchaguliwa kea usimamizi mzuri wa lishe kwa kuwa watoto wote wanapata chakula katika shule zote za Wilaya ya Maswa.
“Nichukue nafasi hii kuwashukuru watendaji wa Kata, Vijiji na viongozi wengine mliochini kwa kubadilika na kuanza kuwa wabunifu na kufanya kazi vizuri kwa kuwa kazi inaonekana kwenye usimamizi na ufuatiliaji wa afua za lishe.” Mhe Kaminyoge
Pia amewataka Watendaji hao kuhakikisha wanaangalia namna ya kuwasaidia watoto ambao wanatoka katika familia ambazo hazina uwezo wa kupeleka chakula shuleni ili na wao wasijisikie sehemu ya familia vibaya kwa lengo la kuwafanya waendelee kusoma
Wale watoto wengine wanajiona kama yatima tunatengeneza kitu kingine ambacho kikubwa kwa wale watoto wenzao wakinywa uji wanapoingia darasani na wenyewe hawajanywa uji ni ngumu sana yule mtoto kuelewa
Pia amesema Watendaji wa Kata wana jukumu la kusaidia watoto ambao hawajiwezi katika maeneo yao kwa kuwachambua watoto wanaotoka katika familia ambazo hazijiwezi ili nao waweze kupata chakula shuleni na kujisikia kama sehemu ya familia kwenye shule wanazosoma.
Aidha ametoa wito kwa watendaji kwa robo ijayo ya tathmini hali ya lishe iwe asilimia 100% wototo wote wapate uji na chakula mashuleni kwa kuwa sasa ipo asilimia 98% ya watoto wote.
"Watendaji kafikilieni watoto ambao wapo wenye hali mbayahawawezi kupata msaada wowotekutoka nyumbani kuleta chakula shuleni wapo mkawabainishe muone namna gani ya kuzungumza na kamati ya shule na serikali ya kijiji muone mnawasaidiaje wale tunaweza tukaweka kundi ambalo linasababisha wasipate elimu nzuri kwa sababu ya kuwabagua kupata uji au chakula shuleni." Mkuu wa Wilaya
Aidha ametoa wito kwa watendaji wa kata kwa robo ijayo ya tathmini hali ya lishe iwe asilimia 100% ya watoto wote wapate uji na chakula mashuleni kwa kuwa sasa ipo asilimia 99% ya watoto wote wanaopata chakula shuleni.
Katika hatua nyingine ametoa pongezi kwa watendaji wa Kata kwa kusimamia kwa ufanisi ugonjwa wa kipindupindu ulikuwa umejitokeza katika kwa kudhibiti kwa siku 18 na baada ya siku 30 Wilaya y a Maswa haikuwa na ugonjwa wa kipindupindu tena.
Aidha ametoa wito kwa watendaji kuendelea kuchukua tahadhari kwa kutoruhusu wananchi kula katika chakula kwenye mikusanyiko kwa kuwa ugonjwa huo Bado upo katika wilaya za Itilima, Bariadi na Meatu.
"Niwaombe matukio hayo yakitokea kwenye Kata zenu muwaambie wenyeviti wa vitongoji, wenyeviti wa Kijiji na watendaji wa vijiji kwamba hakuna tena kula kwenye mikusanyiko mpaka mtakapotangaziwa kwa sababu kama kipindupindu kipo Itilima, Bariadi na Meatu ni rahisi kufika kwetu sisi na chenyewe hakichagui mipaka." Amesema Mhe. Kaminyoge
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.