Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge amekutana na wananchi wa Kata ya Jija kwa ajili ya kuwahamasisha kujiandikisha katika dafatari la mkazi ili waweze kupata haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika 27 Novemba 2024.
Mkuu wa wilaya amesema hayo wakati akizungumza na wananchi katika Gulio la Jija ambapo amewaeleza wananchi tofauti ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura na zoezi la uandikishaji wa orodha ya daftari la mkazi.
“Zoezi ninalowahamsisha na kuwaelimisha ni zoezi ambalo wananchi wote wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea wakajiorodheshe kwenye vituo vya mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa mwezi ujao wa tarehe 27, Novemba 2024.” Amesema Mhe. Kaminyoge
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.