Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge amekutana na viongozi wa AMCOS katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa ajili ya kuwahamasisha kujiandikisha katika orodha ya daftari la wapiga kura ili waweze kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Pia Mkuu wa WIlaya ametoa wito kwa viongozi hao kwende kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi waendelee kujiandikisha kwenye orodha ya daftari la mkazi ili wasikose haki yao ya msingi ya kuwachagua viongozi ambao watapeleka maendeleo katika maeneo yao.
Zoezi la uandikishaji wa orodha ya daftari la wapiga kura wa serikali za mitaa lilianza tarehe 11, Oktoba 2024 na linatarajiwa kumalizika tarehe 20 Oktoba 2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.