Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Aswege Kaminyoge amesema serikali ya awamu ya sita ya Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika huduma za kijamii na kiuchumi ambapo kuanzia marchi 2021 mpaka sasa Wilaya ya Maswa imenufaika na miradi ya bilioni 30 mpaka 40.
“Fedhe hizo zinatolewa kwa ajili ya kumalizia miradi ambayo wananchi wameanza nayo hivyo amewataka viongozi wa Vijiji, Kata na Chama kutoa elimu kwa wananchi mahali penye upungufu wa vyoo wananchi wasaidie kuchimba na kujenga ili hela zinazotolewa na Mhe Rais ziweze kumalizia kazi hizo kwa ajili ya ufundi na vifaa vya viwandani.
Mhe Kaminyoge amesema hayo wakati akijibu kero mbalimbali zilizotolewa na wananchi katika ziara ya mwenyekiti wa ccm mkoa wa simiyu alipotembelea wilayani maswa kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero la wananchi pamoja na kufatilia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 -2025 katika tarafa zote za Wilaya Maswa
“Mhe Rais kwa mwaka huu unaoisha juni ametoa shilingi milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo laiti kama katika wilaya hii ya maswa shule za msingi na shule za sekondari zingekuwa tayari na matundu yaliyojengelewa tungeweza kutumia shs 300 zote kukamilisha upungufu wote wa vyoo ambavyo tunavihitaji kwa sasa.” Mkuu Wa Wilaya
Pia amewataka viongozi kutoa elimu kwa wananchi ili serikali imalizie pale wananchi walipoiishia vilevile Mhe Rais katika mwaka wa fedha uliopita alitoa zaidi ya shs bilioni 5.5 kwa ajili ya kumalizia vijiji 39 ambavyo havikuwa na umeme katika wilaya
Mkuu wa Wilaya amesema Mhe Rais ametoa maelekezo ifikapo 2025 atatoa fedha nyingine kwa ajili ya kusambaza umeme mpaka ngazi ya kitongoji hivyo amewataka wananchi kuwa na subira kwa kuwa serikali inaedelea kuchakata ili ifikapo 2025 vitongoji vyote viwe na umeme nchi nzima.
Mkuu wa Wilaya pia ameendelea kutoa wito kwa viongozi kuendelea kusikiliza na kutatua kero za wananchi sambamba na hilo katika kuboresha miundombinu ya maji Mhe Rais ametoa zaidi ya shs milioni 600 katika kijiji cha Mwashegesi kwa ajili ya kusambaza maji kwa wananchi,
ametoa bilioni 1.9 kwa ajili ya tenki kubwa katika Kata ya Zanzui ili maji yasambae Zanzui, Malita na Mwabujiku, Mwamashimba ametoa zaidi ya bilioni 1.9, Hinduki Kata ya Sukuma ametoa zaidi ya bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa tenki kubwa kwa ajili ya kusambaza maji mjini na Ngongwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.