Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Mhe. Aswege Kaminyoge ametoa wito kwa viongozi wote kuhakikisha wanasimamia watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule kuanzia awali, msingi na sekondari waandikishwe kwa ajili ya kuanza masomo kwa kuwa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa Fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya.
Ametoa wito huo katika kikao cha baraza la Madiwani robo ya kwanza ya mwaka 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, wataalamu pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya.
Mhe Kaminyoge amesema jukumu hilo la msingi wamepewa maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na vijiji kuhakikisha wanawatumia viongozi wa vitongoji kwa kuwa wao ndio wana majukumu mahususi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanaenda.
Mkuu wa Wilaya amewahimiza na kuwasisitiza waheshimiwa Madiwani na viongozi kuwasisitiza wananchi watoto wote walioandikishwa kuanzia awali, msingi na sekondari wanasimamiwa kikamilifu ili kuhakikisha wanamaliza elimu zao.
"Mhe Rais tangu aingie madarakani hakuna mwananchi yeyote amepitiwa juu ya uchangiaji wa miundombinu Jija Mhe Rais ametoa milioni 548 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi yenye darasa la awali na mikondo 2 kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba yenye madarasa 17". Amesema Mhe. Kaminyoge
Pia Mhe Kaminyoge amesema wataanzisha oparesheni kwa kuwatumia Maafisa Tarafa, Watendaji kuhakikisha watoto wote waliopo nyumbani ambao wamefikia umri wa kwenda shule wanaenda ili kumheshimisha Mhe Rais ambaye ametoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na shule mpya.
Pia Mkuu wa Wilaya amesisitiza Madiwani kusimamia mapato ya Halmashauri ili kufikia lengo la makusanyo ifikapo Juni 2024 iwe ni asilimia 100% usimamizi wa asilimia 40 ya mapato ya Halmashauri itume kama ilivyopangwa.
Ikiwa asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na 30% katika miradi ya maendeleo pamoja na taarifa za afua za lishe ziwepo kwenye taarifa za Kata kwa kuwa viongozi wamesaini mkataba ili kutekeleza mpango huo wa lishe kwa akina mama wajawazito kupata madini chuma na watoto chini ya miaka 5 kuepuka udumavu.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Budekwa Mhe. Esther Ng'holongo kwa niaba ya Madiwani wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kazi kubwa anayoifanya na ameahidi kushirikiana nae katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.