• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Mrejesho |
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini ya Mjini
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Uratibu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Tehama
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria ndogo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

DC asisitiza wakulima wote wapatiwe mabomba

Posted on: March 3rd, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge ameagiza wakulima wote waliolima pamba  wanatakiwa kupewa mabomba kwa ajili ya kunyunyizia sumu katika mashamba yao ya pamba kuepukana na wadudu kuharibu mazao.

Mhe Kaminyoge amezungumza hayo katika baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Maswa katika kikao cha robo ya pili mwaka wa fedha 2022/2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wakati akitoa salamu za serikali.

Mkuu wa Wilaya amesema kuwa mwaka huu AMCOS imenunua pamba kutoka kwa wananchi ambapo kupitia fedha hizo Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imenunua bomba ambazo zimegawiwa katika vijiji 120  kwa ajili ya kuwagawia wakulima pamoja na bodi ya pamba Tanzania ambayo imetoa bomba za kunyunyizia sumu na viuatilifu.

Mhe. Kaminyoge ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hasan kwa kutoa viuatilifu bure ambavyo ni vizuri kwa kuwa vinaua wadudu na vina ubora.

Ameongeza kuwa wakulima wote waliolima heka kuanzia 10 na kuendelea wenye uwezo wa kuuza mifugo yao kama vile mbuzi  wanunue mabomba yao wenyewe kwa ajili ya kupulizia mashamba yao ya pamba kuliko kusubiri bomba la kuazima kwa sababu mkulima akimiliki bomba lake mwenyewe litamsaidia mkulima  kunusuru pamba yake na kupata mavuno mazuri.

Amesisitiza kwa kumwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kutoa waraka / mwongozo ambao utamfanya kila mkulima aliyelima pamba aweze kupata bomba hizo kupitia watendaji wa vijijini ambao watashirikiana na  kamati za vijiji kujua idadi kwa ajili ya kukabidhi kwa wenyeviti wa vitongoji ili waweze kuwapa wananchi wao kutumia katika kupulizia mashamba yao.

Pia Mhe. Mkuu wa Wilaya ametoa onyo kwa wananchi au maduka binafsi yanayouza viuatilifu kuwa yeyote atakayekutwa anauza viuatilifu hivyo madukani na mnadani  hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na hakutakuwa na dhamana kwake kwa kuwa atahesabika kama mhujumu uchumi.

Aidha,  Mhe. Kaminyoge amewasisitiza waheshimiwa madiwani kufanya mikutano kwa kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hasan imejitangaza yenyewe kwa kutekeleza miradi Mikubwa ya kati na midogo hivyo ni jukumu la viongozi kuwaeleza wananchi jinsi serikali ilivyofanya na inavyoendelea kufanya kazi.


Matangazo

  • TANGAZO LA UHAMASISHAJI CHANJO YA MIFUGO January 21, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI May 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI May 27, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO May 30, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA YATOA MAFUNZO YA MFUMO WA NeST KWA WATAALAMU WA UNUNUZI WILAYANI MASWA

    March 27, 2025
  • DKT ANNEY; NENDENI MKASIMAMIE MIRADI YETU VIZURI

    March 26, 2025
  • VIKUNDI 15 VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYAPATA MKOPO

    March 26, 2025
  • KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO MASWA

    March 10, 2025
  • Tazama zote

Video

Fursa za uwekezaji Mkoani Simiyu
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Sensa ya mwaka 2022
  • Taarifa ya Mapato na matumizi
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa IMIS
  • Mfumo wa PlanRep
  • Government Web Framework
  • Mfumo wa PREM
  • Maswa DC Mail Domain
  • Hotuba ya Mh. Waziri Mkuu PLANREP/FFARS

Viunganishi linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Sekretariet ya Ajira
  • Ikulu
  • Baraza la Mitihani Tanzani
  • Wizara ya Elimu Tanzania
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

    Sanduku la Posta: 170, MASWA

    simu ya Mkononi: +255 282 750 271

    Simu: +255 282 750 271

    Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.