Katibu Tawala wa Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Ndg Athuman Kalaghe amezindua mfumo wa stakabadhi ghalani ambao utamsaidia mkulima kupata faida kwa kuwa atauza kulingana na bei iliyopo sokoni.
Ametoa maagizo hayo katika uzinduzi wa mfumo wa stakabadhi ghalani uliofanyika leo tarehe 13 march 2024 katika maghala yaliyopo Sola na kuhudhuliwa na makatibu wa AMCOS Mrajisi mkuu wa Mkoa mkoa wa Simiyu, Mwenyekiti wa vyama vya AMCOS Mkoa wa Simiyu
"Mara nyingi tumekuwa tukipoteza mapato mengi ususani kwenye zao la choroko kwa sababu zao letu la choroko limekuwa likitoroshwa kutoka nje ya mipaka yetu ya Wilaya kwa hiyo tunajikuta Halmashauri yetu ya Wilaya tunakosa mapato.” Amesema Ndg Kalaghe
Katibu Tawala amesema Lengo la kutumia mfumo huo ni kuwa na takwimu sahihi za ukusanyaji wa mazao ili kuwezesha serikali kukusanya mapato yake kwa usahihi kwa kuwa takwimu sahihi zikiwepo zitaisaidia Halmashauri kupata mapato mengi.
Pia ameongeza kuwa mfumo huo utampatia mkulima bei nzuri iliyopo sokoni sasa na kumuwezesha kupata faida pamoja na serikali pia itapata faida kutokana na matumizi ya mfumo huo.
Pia ametoa wito kwa makatibu wa AMCOS waliochaguliwa kuwa waadilifu kwa kuwa wao ndio chanzo cha kufaidika kwa mkulima aliyepo kijijini kwa kuwa Maswa wanaweza kutumia mfumo huo.
“Uadilifu ndio jambo kubwa sana kwa makatibu wa AMCOS tukitaka Wilaya yetu itulie uandilifu wenu kwenye kazi , kwenye ukusanyaji wa choroko tusimraghai mkulima kule kama bei imepanda tununue kwa bei iliyopanda sio bei ni 1100 wewe unakwenda kununua 600 ndio maana wengine wanakata tamaa.” Ndg Kalaghe
Mhe Kalaghe amesema serikali ya awamu ya sita inataka mkulima afaidike kwa kuwa stakabadhi ghalani ndio njia pekee iliyomtengenezea mkulima aweze kupata mafanikio na serikali itapata mapato yake kwa urahisi na kujua takwimu sahihi za mzigo au mazao yaliyokusanywa kutoka kwa wakulima.
“Mkulima anasubiri anaangalia kile kitakachouzwa kitakachozidi je? atarudishiwa kama tulivyoahidi? kwa hiyo ndugu zetu wakulima wa maswa wanasubiri kuona hilo sasa watakaporudishiwa kile ambacho kimezidi ndio utaona ghala hili litajaa tulipanga tukusanye tani elfu sitini lakini mpaka sasa tuna tani elfu 50.” Katibu Tawala
Nae Mwenyekiti wa AMCOS Mkoa wa Simiyu Ndg lazato Walwa ameishukuru Wilaya ya Maswa kwa kupokea malalamiko na kuyapatia ufumbuzi kwa kujikita katika kutafuta masoko ambapo zaidi ya tani 50 zimekusanywa na AMCOS kwa ajili ya mnada kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani.
“Nitoe shukrani zangu kwa Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji na safu yotekwa maana kipekee kabisa waliweza kuona hii ni fursa kwa vijana wao ambao wapo ndani ya Maswa lakini pia ni fursa kwa sisi ambao ni wakulima kwa maana ya mazao yetu.”
“ tunaweza kuangalia ni kwa namna gani kabla hatujaingia kwenye soko kama chama kikuu yalikuwa kwenye level gani mara baada ya kuingia kwenye soko yalienda kwenye level gani niwashukuru TMX kwa kuwa wameweza kutuunganisha na wafanyabiashara wakubwa ambao kupitia soko la kimtandao tunaona juhudi zinazofanyika kwa kuona namna ya kupanda kwa soko la choroko.” Amesema Ndg Walwa
Katika wilaya ya Maswa vyama 11 vya AMCOS vimepewa dhamana ya kukusanya mazao kwa ajili ya kupeleka ghala kuu ambapo mnada utakapofanyika kupitia mfuko wa stakabadhi ghalani.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.