Katibu Tawala Wa Wilaya ya Maswa Ndg Athuman Kalagwe amezindua mafunzo ya usambazaji wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi kwa watendaji na viongozi mbalimbali yenye lengo la kuwajengea uwezo kutumia matokeo ya sensa ili yawasaidie katika kutekeleza majukumu yao kwa makini na ubora zaidi katika sera ya upangaji wa mipango.
Amezungumza hayo katika kikao cha mafunzo ya usambazaji wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa pamoja na wadau mbalimbali yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
ameongeza kuwa Wilaya ya Maswa imejipanga kuhakikisha mipango na programu zote za maendeleo zinapangwa kwa kuzingatia matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
“katika program zetu na mipango ya bajeti ya mwaka 2023/2024 imezingatia matokeo ya sensa na takwimu zingine zinazozalishwa na ofisi ya taifa ya takwimu baada ya kutekeleza maelekezo ya serikali Wilaya yetu imeweka msisitizo wa matumizi ya matokeo ya sensa kwa lengo la kuhakikisha mipango na program hizo zinajibu changamoto mbalimbali.” Amesema Katibu Tawala
Katibu Tawala ameongeza kuwa Halmashauri ya Maswa ina idadi ya watu 427,864 ambapo wanaume 28,255 na wanawake ni 21,9906 ambapo ongezeko la watu ni sawa na asilimia 2.2%.
amesema wananchi wanatakiwa wapate huduma stahiki kwa wakati na zenye ubora zinazozingatia mahitaji harisi ya wananchi kulingana na idadi yao, jinsia yao na kuzingatia mahitaji maalumu ya makundi mbalimbali katika jamii na hali ya mazingira wanapoishi.
“Mafunzo haya kwetu ni muhimu sana kwa sababu yanatujengea uwezo wa kuyatafsiri na kuyatumia matokeo ya sensa ipasavyo na hatimaye kukuza Uchumi wa Halmashauri yetu, kuongeza upatikanaji wa huduma za jamii kwa wananchi na kuchagiza harakati za wananchi kwa kupambana na maadui watatu ambao ni ujinga ,maradhi na umasikini.” Ndugu Kalaghe
Katibu Tawala amesema takwimu hizo zimekuja kisayansi kwa kuwa zitasaidia viongozi mbalimbali katika mahitaji mbalimbali katika Kata husika kuangalia namna gani maendeleo yatafanyika.
"Hii ni njia moja ya kisayansi ya sisi kuweza kuleta maendeleo kwenye Wilaya yetu leo hii hatutegemei Mtendaji wa kata tukwambie hebu tuletee Kata yako wangapi hawana choo ukashindwa, hatua gani umechukua ukashindwa wakati kila kitu kinajieleza kwa kuwa kila kitu kimewekwa kisayansi." Katibu Tawala
Pia amesema takwimu hizo ni kipimo kwa watumishi kwa kuwa wamerahisishiwa na watakuwa na uwezo wa kutatua changamoto hizo na Wilaya haitakuwa na shida kabisa.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali Ndg Benedict Mgambi amesema mafunzo hayo ni mfululizo wa mafunzo yatokanayo na matokeo ya sensa ya watu na makazi kwa makundi mbalimbali katika jamii.
Pia amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango kazi wa usambazaji wa mafunzo ya matumizi ya matokeo ya watu na makazi ya mwaka 2022 ambapo hadi sasa mafunzo kama hayo yamefanyika kwa makundi mbalimbali mpaka ngazi za chini.
Mafunzo hayo yatahusisha viongozi wa siasa, dini, mira na desturi asasi za kiraia sekta binafsi, taasisi za elimu ya juu, watu wenye ulemavu, waandishi wa Habari na wananchi wa kawaida.
ameongeza kuwa madhumuni ya kusambasa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ni kuwajendea uwezo wadau wote kwa namna ya kutumia matokeo hayo katika kutekeleza majukumu yao ya uongozi na utendaji katika serikali kuu na mamlaka za serikali za mitaa.
“kufanya hivyo kutasaidia kuongeza uwazi na kupanua wigo wa matokeo ya matumizi ya sensa kwa serikali, sekta binafsi na wananchi kwa ujumla ili kupanga mipango jumuishi kwa maendeleo endelevu.” amesema Mgambi
wa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg Maisha Mtipa amemshukuru Rais kwa kuweza kuwezesha zoezi la sensa kuanzia mpango, wakati wanachukua taarifa kwa kuwa taarifa zimechakatwa na kuletwa katika level ya chini kabisa kwa watendaji wa vijiji.
Pia amewataka viongozi wote kuanzia waheshimiwa madiwani,maafisa tarafa , watendaji wa kata na vijiji kila mmoja apate taarifa hizo kwa ajili ya kufanyia kazi ili kuleta maendeleo ambayo serikali inayahitaji kwa kuwa mipango yote inaanzia ngazi ya chini
“Tutakapokuwa tunapanga mipango ya Kijiji takwimu hizi zitatuonyesha watu, huduma muhimu za jamii na mambo mengine yaliyoonyeshwa nitoe wito kwa kila mmoja wetu aliyepo hapa tutumie hizi takwimu kwa ajili ya kuleta maendeleo ya nchi yetu.” Amesema Ndugu Mtipa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.