Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Aswege Kaminyoge amekabidhi madawati 100 katika shule za msingi na viti na meza 200 katika shule za sekondari wilayani Maswa vyenye thamani ya shs milioni 18 zilizotolewa na Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa lengo la kupunguza changamoto ya madawati katika shule zenye upungufu huo.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 23 April 2024 katika chuo cha ufundi stadi Binza kilichopo Njiapanda ya Lalago Maswa ikiwa ni sehemu ya kuelekea sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Tanzania.
Mkuu wa wilaya amewapongeza Wakuu Wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa baada ya kuona changamoto ya ubungufu wa madawati uliopo na kutoa fedha za matumizi ya shughuli za ofisi zao kwa ajili ya kutengeneza madawati ambayo yatakabidhiwa katika shule zenye upungufu mkubwa.
Pia amezitaka taasisi zingine za serikali TARURA, RUWASA, MAUWASA na taasisi za kifedha vikundi na watu binafsi kuiga mfano huo kwa kutoa mchango kwa jamii wanapofanyia kazi ili watoto wapate madawati na kupunguza tatizo hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Binza Mwalimu Mabula Daniel amesema Chuo hicho kinatoa kozi mbalimbali ikiwepo kozi ya uselemala hivyo chuo kilipokea shs milioni 18 kutoka Timu ya Menejimenti kwa ajili ya kutengeneza madawati seti 100 kza shule za msingi na seti 200 kwa shule za sekondari ambayo yapo tayari kwa matumizi.
Pia Mwalimu Mabula amesema huo ni mwendelezo wa mpango wa kutengeneza madawati 430 na kazi inaendelea pia ametoa wito kwa taasisi zingine na watu binafsi kujitokeza kuiunga mkono halmashauri ili kusaidia kuondoa tatizo la upungufu wa madawati katika Wilaya ya Maswa.
Kwa upane wake mkuu wa Divisheni ya elimu sekondari Fidelis Apolinary amesema amepokea viti na meza 200 ambavyo vitagawiwa katika shule zenye upungufu wa madawati ambazo ni shule ya sekondari nyongo ambayo imepata vitio na meza 100 na shule ya sekondari mwasayi 100.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.