Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Maswa amekabidhi mapipa 40 ya kutupia taka kwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ikiwa ni lengo la kuchangia nyenzo za kuwezesha kuuweka mji wetu wa Maswa kuwa safi.
Chini ya usimamizi wa Afisa Afya na Mazingira wa Wilaya vifaa hivyo vya kutunzia taka vimekabidhiwa kwa Wenyeviti wa Vitongoji vya Mjini hapa ili kuweka maeneo yao katika hali ya usafi. Kila raia anaagizwa kuweka mazingira katika hali ya usafi kwa kutupa au kuweka takataka eneo stahiki.
Acha kutupa taka ovyo weka sehemu inayohusika ili kuweka mazingira yetu katika hali ya unadhifu.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.