Balozi wa indonesia amekuwa na ziara ya siku moja Wilayani Maswa ambapo ameweza kutembelea kiwanda cha kusindika bidhaa za ngozi kilichoko senani, pia amefanikiwa kutembelea kiwanda cha chaki kilichoko Maswa mjini. Aidha amepata taarifa za uwepo wa kiwanda cha kusindika bidhaa za mchele kilichoko mjini Malampaka na kiwanda tarajali cha unga wa viazi lishe kinachojengwa Njiapanda.
Akihutubia wananchi wa kata ya Senani Wilayani hapa amesema ushirikiano kati ya Indonesia na Simiyu hasa kwenye kilimo na viwanda atasaidia usindikaji wa bidhaa za ngozi, kuleta wataalamu kutoka Indonesia na kuwapeleka wataalamu/watu kutoka huku kwenda kusoma.Ushirikiano wa Nchi ya Indonesia na Tanzania ulianza mwaka 1965. Mkataba wa ushirikiano baina ya Mkoa wa Simiyu na Indonesia utasainiwa hivi punde.
Akiwa Maswa akiangalia fursa za kiuchumi amesema ataweza kuchukua Pamba na kuisafirisha kwenda Indonesia.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.