Saturday 15th, March 2025
@
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa inaendelea na semina ya uandaaji wa mpango mkakati wa miaka mitano baada ya uliokuwa ukitumika kuisha muda wake. Wakuu wa Idara na Vitengo wakishirikiana na watushi wengine chini ya Wataalamu washauri kutoka Chuo cha Mipango Dodoma wamefikia siku ya pili sasa. Kesho tarehe 24/11/2017 kutakuwa na kikao cha Wadau wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa ajili ya kutoa maoni na kuchangia masuala mhimu ya maendeleo ili yajumuishwe kwenye mpango mkakati huo. Hivyo kila mdau anakaribishwa Ukumbi mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kuanzia saa 2.00 asubuhi ili kuandaa mambo ya mhimu kutekelezwa ili kujenga Maswa yetu.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.