Friday 17th, January 2025
@
Mwenge wa uhuru Wilayani Maswa utapokelewa kutoka Wilaya ya Busega tarehe 19/8/2018 na kukimbizwa katika vijiji vyake.
Shamrashamra za mapokezi zitakuwa katika kijiji cha Jija kata ya Jija.
Mwenge utafungua miradi mbalimbali ya maendeleo, kukagua shughuli za vikundi mbalimbali katika vijiji vya kata za Jija, Malampaka, Binza, Nyalikungu na Shanwa.
Vijiji vitakavyopitiwa na Mwenge ni kama ifuatavyo: Jija, Mwatumbe, Shishiyu, Mwaliga, Igwata, Mwanhegele, Mwabagalu, Nyabubinza, Lali, Malampaka, Bukigi, Gulung'washi, Bukangilija, Nhelela, Njiapanda, Isulilo, Busamuda,Sayusayu, Binza, Nyalikungu na Shanwa.
Mkesha utafanyika katika uwanja wa nguzo nane mjini Maswa. Katika mkesha kutakuwepo na bendi ya kutumbuiza.
Wananchi wote mnakaribishwa kushangilia katika maeneo yenu na katika mkesha uwanjani nguzo nane.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.