Wakuu wa Idara na Vitengo wamefanya ziara ya kutembelea Miradi ya maendeleo hapa Wilayani. Miradi iliyotembelewa ni ya Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa pamoja na matundu ya Vyoo katika Vituo vya kutolea huduma ya Elimu na Afya.
Ziara hiyo imefanyika katika Kata ya Masela, Mwabaratuku, Busilili, Mbaragane, Lalago, Dakama, Sangamwalugesha, Senani, Mwamanenge, Zanzui na Sola.
Miradi hiyo iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Viongozi hawa wametoa maelekezo mbalimbali katika kila kituo kutokana na yaliyojitokeza au kubainika kulingana na hatua mradi ulipofikia huku wakisisitiza ukamilishaji wake ufanyike mapema ili ianze kutumika.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.