Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Miriam Mbaga ametembelea Wilaya ya Maswa leo. Amefika kuona shughuli zinazoendelea, kukutana na Watumishi wa Umma na Viongozi mbalimbali katika Tarafa.
Ametambelea eneo la uwekezaji ambapo ameona ujenzi wa Kiwanda cha Mikate ulioko katika hatua ya msingi.
Amekutana na Watumishi wa Umma na Viongozi mbalimbali wa Tarafa ya Mwagala Wilayani hapa katika Shule ya Msingi Lalago Ufundi iliyoko Kata ya Lalago. Amewahasa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufanikisha shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Amewasisitiza kila mmoja kusimamia suala zima la ukusanyaji wa mapato ya ndani. Aidha Viongozi nagzi ya vijiji wamehaswa suala zima la utoaji wa taarifa ya mapato namatumizi kwa jamii ili kuleta uwazi na uaminifu.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.