Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa akiongozana na Wakuu wa Idara na Vitengo leo tarehe 4/11/2019 ameongea wa wazazi, walezi na Waalimu wa Shule ya Msingi Nyalikungu.
Lengo kuu la mazungumzo lilikuwa ni kuongelea suala la uboreshaji wa miundombinu ya Shule ili kuweka mazingira mazuri ya watotot kujifunza.
Shule hii ina Jumla ya Wanafunzi 1415, idadi ya vyumba vya madarasa 12 pungufu ni 24, Idadi ya Walimu 25, Idadi ya Nyumba za Walimu 2 pungufu 23, Idadi ya matundu ya vyoo 8 pungufu 49 na ina upungufu wa madawati 100.
Pamoja na upungufu wa miundombinu iliyopo shule inafanya vizuri, mwaka huu 2019 imekuwa ya 4 kiwilaya matokeo ya darasa la Saba.
Katika mazungumzo hayo wamekubaliana mchango wa kuchangia uboreshaji miundombinu wa kuanzia Sh. 10,000/= kila mzazi kwa awamu mbili yaani ndani ya wiki 2 sh. 5,000/= iwe imelipwa na hadi kufikia mwezi Desemba Sh. 10,000/= iwe imekalika.
Baadhi ya Wazazi na Walezi wameanza kutoa michango yao palepale na kiasi cha fedha Taslimu Sh. 1,029,000/= zimekusanywa. Ahadi zilizopatikana ni mifuko 11 ya Saruji na Fedha Sh. 740,000/=.
Aidha wamemhaidi Mkurugenzi kuwa kufikia tarehe 6/12/2019 kila mzazi au mlezi atakuwa ameisha kamilisha mchango wake hivyo na Halmashauri kutoa mchango wake pia.
Kwa pamoja tushirikiane kuijenga Maswa.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.