Uzinduzi wa Bodi ya Kampuni ya Viwanda ya Ng'hami ( Ng'hami Industries Company Limited ) inayomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa umefanyika tarehe 12/08/2020 katika ukumbi Mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa. Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa Watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo ESRF, UNDP, ADB Bank, NMB Bank n.k.
Bodi hii ina jumla ya Wajumbe sita ambao ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Fedha, TAMISEMI, Mtaalamu wa Viwanda, Mdau kutoka katika kijiji cha Njiapanda, Mdau mwanzilishi wa Kampuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambaye ndiye Mwenyekiti. Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege E. Kaminyoge.
Siku imeanza kwa Wajumbe wa Bodi kutembelea Viwanda vyote vinavyofanya kazi na ambavyo havijaanza kazi.
Kwa uzinduzi huu hatimaye Maswa ya Viwanda imeanza kusonga mbele.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.