Halmashauri ya Wilaya ya Maswa katika hatua ya kuinua uchumi wa wananchi na pato lake imethubutu kusimamia uanzishwaji wa viwanda mbalimbali ikiwa ni hatua ya kutekeleza maelekezo ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dr. John Pombe Magufuli.
Viwanda hivyo ni kiwanda cha Chaki, kiwanda cha kusindika bidhaa ya ngozi ( Viatu, mikanda n.k), kiwanda cha kukoboa na kupanga madaraja mchele na kiwanda cha viazi lishe. Sambamba na hili iko katika hatua ya kuanzisha viwanda vikubwa mbalimbali.
Ikiwa katika utekelezaji wa majukumu yake Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM) imetembelea kiwanda cha kusindika Viazi lishe kilichopo katika kijiji cha Njiapanda Kata ya Isanga wilayani hapa. Kiwanda hiki kimeanzishwa kwa lengo la kupunguza utapiamlo, kuboresha afya na kuongeza kipato kwa jamii. Kiwanda hiki kilianza kujengwa tarehe 22/1/2018 na kuanza uzalishaji tarehe 2/8/2019.
Kiwanda kimeanza kufungasha mifuko ya Kg.1 ya unga wa viazi lishe. Gharama ya Kg.1 ya unga uliofungashwa ni Tsh. 4500/= bei ya jumla kiwandani na Tsh. 5000/= bei ya rejareja. Unga huu unatumika kupikia uji, chapati, maandazi, mikate n.k kwa kuchanganya na unga wa ngano. Pia unatumika kama kiungo kwa ajili ya kuongeza viinilishe katika chakula kama chai, uji, maharage, makande, ndizi n.k
Makundi rika yote yanahamasishwa kutumia unga huu kwa ajili ya kuboresha afya zao.
Katika ziara hiyo Kamati ya FUM imeweza kutembelea pia Ujenzi wa Wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa, Mradi wa maji wa Jihu Ikungu, Mradi wa Maji wa Nyashimba Mhida na Ukamilishaji wa Zahanti ya Wigelekelo.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.