Idara ya fedha ni miongoni mwa idara za Halmashauri ya Wilaya zinazounda timu ya menejementi ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambayo inalojukumu la kutoa huduma bora mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa wananchi na wadau wake. Idara ya fedha inalo jukumu la msingi la kusimamia mapato na matumizi ya fedha za Halmashauri jukumu hili limejengwa na kusimamiwa pia na sheria mbalimbali zinazoongoza utendaji kazi wa kila siku kwa kutumia sheria ya fedha namba 6 ya mwaka 2001 na marekebisho yake ya mwaka 2004,Sheria ya fedha ya serikali za mitaa CAP 290 ,Sheria ya bajeti ya mwaka 2015, Mwongozo wa fedha wa serikali za mitaa wa mwaka 2009 (The Local Authority Financial Memorundum of 2009) ,Sheria ndogo za Halmashauri pamoja na miongozo na nyaraka mbalimbali za Serikali zinazosimamia taratibu za fedha.
Katika kutekeleza majukumu yake Idara ya Fedha imegawanyika katika vitengo vikuu kama ifuatavyo:
Kitengo cha Mapato
Kitengo cha Matumizi
Kitengo cha Ufungaji hesabu za mwisho (Final Accounts)
Kitengo cha Mishahara
Kitengo cha Biashara
Kitengo cha Mapato
Kitengo hiki kinasimamia shughuli zote za ukusanyaji wa mapato kwa kushirikiana na Idara zenye vyanzo mbalimbali vya mapato kulingana na bajeti ya Halmashauri ya Mji.
Kinasimamia mfumo wa ukusanyaji mapato ya Halmashauri wa kieletroniki (Local Government Revenue Collection information system-LGRCIS) kwa kufanya yafuatayo:
Kutoa stakabadhi za kukiri mapokezi
Kutunza kumbukumbu zote za vyanzo vya Mapato ya Halmashauri
Kuandaa na kutoa taarifa za makusanyo ya mapato ya Halmashauri kwa mwezi,Robo mwaka na Mwaka mzima.
Kitengo cha Matumizi
Kitengo hiki kinasimamia shughuli zote zinazohusiana na malipo ya fedha za Halmashauri kama vile:
Kuandaa hati za malipo mbalimbali ya Watumishi,wazabuni,na taasisi mbali mbali zilizotoa huduma kwa Halmashauri .
Kusimamia na kutumia mfumo wa malipo wa kielectroniki (IFMS-EPICOR SYSTEM)
Kutunza kumbukumbu za malipo yote yanayofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Kitengo cha Mishahara
Kitengo hiki kinashughulika na masuala ya urekebishaji na ulipaji wa mishahara ya watumishi kwa kushirikiana na idara ya Utumishi
Kusimamia malipo yanayofanana na ajira kwa watumishi wa muda mfupi hasa wanaolipwa kutokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Kitengo cha Ufungaji wa Hesabu za Mwisho (Final Financial Statements)
Kitengo hiki kinahusika na kuandaa taarifa za fedha za mwaka za Halmashauri (Final Financial Statements)
Kuandaa na kuweka vizuri kumbukumbu zote zinazohusiana na hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Kitengo cha Bihashara
Kitengo hiki ni maalumu kwa ajili ya kusimamia shughuli zote za biashara katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kama vile:
Utoaji leseni zote za kibiashara
Kutoa ushauri katika masuala ya biashara
Usimamizi wa masuala ya utekelezaji wa sheria ya leseni za biashara ya Mwaka 1972
Majukumu ya Afisa Bihashara
Kuratibu na kusimamia masuala yote ya biashara katika Halmashauri.
Mshauri Mkuu wa masuala ya Sheria za Biashara katika uendeshaji wa biashara.
Mratibu na Msimamizi wa shughuli za utoaji na ukaguzi wa leseni za biashara.
Kuandaa taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za sehemu ya Biashara kwa mwezi,robo na mwaka.
Kuandaa Mpango kazi na bajeti kwa Sehemu ya Biashara.
Kutoa tafsiri ya Sheria na miongozo ya maswala ya Biashara kutoka Serikali Kuu kuja Halmashauri.
Kusimamia kwa karibu na kutoa ushauri wa kitaalamu katika eneo la sekta isiyo rasmi.
Kuratibu, kukusanya na kutunza taarifa na takwimu zinazohusu masuala ya biashara.
Kusimamia utekelezaji wa shughuli za uendeshaji wa biashara na kuhakikisha kwamba viashiria vya utekelezaji vianafikiwa.
Utoaji wa leseni za usafirishaji abiria kwa kutumia pikipiki (bodaboda na bajaji) kwa mujibu wa SUMATRA.
Kufanya usajili wa taxi, Bajaji na bodaboda zinazofanya biashara ndani ya Halmashauri.
Kufuatilia utekelezaji wa bei za mafuta zinazotolewa na EWURA
Ufuatiliaji wa bei za mazao katika masoko
Kuratibu maonyesho ya biashara ngazi ya Wilaya.
Kusimamia miradi inayotekelezwa kupitia Sehemu ya biashara.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.